Miili yetu hutoa mawe ya aina gani na tunawezaje kuyazuia? - BBC News Swahili (2024)

Miili yetu hutoa mawe ya aina gani na tunawezaje kuyazuia? - BBC News Swahili (1)

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Mwili una uwezo wa ajabu katika mambo mengi. Na moja ya uwezo wake wa ajabu ni kuzalisha mawe. Wengi wetu tumesikia kuhusu mawe ya figo au vijiwe vya nyongo. Lakini kuna aina nyingine za mawe katika mwili.

Mawe haya hutengenezwa na nini? Na tunawezaje kuyazuia?

Mawe kwenye figo huathiri takribani mtu mmoja kati ya kumi. Huibuka hasa kutokana na kemikali ya kalsiamu na chumvi, ambayo huvuja kutoka kwenye damu hadi kwenye mkojo.

Hizi ni kemikali za asili zinazopatikana katika mimea na wanadamu. Lakini zikiwa nyingi, zinaweza kujikusanya na kuunda jiwe.

Mawe ya figo yanaweza kutofautiana ukubwa, kutoka ukubwa wa chini ya milimita kwa upana hadi sentimita au zaidi. Yanaweza pia kuwa na maumbo tofauti tofauti.

Pia unaweza kusoma

Miili yetu hutoa mawe ya aina gani na tunawezaje kuyazuia? - BBC News Swahili (2)

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Mawe haya husababisha matatizo yanapoziba mirija ya ureta, mirija miwili inayosafirisha mkojo kutoka kwenye figo hadi kwenye kibofu. Ikiwa hilo litatokea, linaweza kusababisha maumivu makali chini ya mgongo, pamoja na kuzuia mtiririko wa kawaida wa mkojo. Na kusababisha maambukizi au mkusanyiko wa mkojo ndani na karibu na figo.

Mawe ya aina nyingine mwilini. Huundwa kwenye kibofu cha nyongo. Mfumo wa kineli ya nyongo hubeba nyongo hadi kwenye utumbo ili kusaidia kuvunja mafuta. Mawe ya nyongo hutokana na kolesteroli au rangi ya nyongo na zinaweza kuunda jiwe moja au mengi.

Mawe ya kwenye figo, kama mawe ya kwenye nyongo huingia kwenye nafasi nyembamba (kama vile mirija ya nyongo), yanaweza pia kusababisha matatizo ya maumivu ya tumbo, maambukizi na homa ya manjano.

Mawe ya aina nyingine

Miili yetu hutoa mawe ya aina gani na tunawezaje kuyazuia? - BBC News Swahili (3)

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Mawe husabaishwa na maji maji ya mwili. Chukulia mfano mawe kwenye koo au mawe ya mate.

Mate huzalishwa na tezi zilizo karibu na sikio, chini ya taya na ulimi. Mara yawapo kinywani, husaidia kulainisha chakula ili kiweze kumezwa, na huo ndio mwanzo wa mchakato mchakato wa usagaji chakula.

Mawe ya mate huundwa na mambo mengi, ikiwa ni pamoja na kalsiamu, magnesiamu, na fosforasi. Mawe ya mate yanaweza kuzuia uzalishwaji wa mate kwenye kinywa, na kusababisha maumivu na uvimbe.

Kutuama kwa mate kunaweza kusababisha harufu mbaya mdomoni au ladha ya mbaya kinywani mwako.

Miili yetu hutoa mawe ya aina gani na tunawezaje kuyazuia? - BBC News Swahili (4)

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Mawe yanaweza pia kupatikana katika tonsillitis. Iko chini katika koo la juu. Tonsillitis ni tishu za lymphoid ambazo ni sehemu ya mfumo wa kinga ya mwili.

Tonsillitis zina mashimo yanayoitwa crypts, ambayo yanaweza kushikilia vipande vya chakula na mate. Matokeo yake ni jiwe la mafindofindo.

Mfindofindo huwa laini na madogo, lakini yanaweza kuwa magumu baada ya muda na pia kuleta matatizo, hasa harufu mbaya ya kinywa au maambukizi ya mara kwa mara.

Vitu vingine katika mwili vyenye kugeuka kuwa mawe ni; kinyesi, kinaweza kikiwa kigumu sana na hutengeneza mawe yanayoitwa coprolite.

Vilevile uchafu kwenye ngozi, ambao hujilimbikiza kwenye kitovu. Pia unaweza kuunda jiwe linalojulikana kama omphalolith.

Kipi cha kufanya kuepuka mawe?

Miili yetu hutoa mawe ya aina gani na tunawezaje kuyazuia? - BBC News Swahili (5)

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Kwa bahati nzuri, kuna hatua rahisi ambazo zinaweza kuzuia mawe haya au kuyaondoa. Jambo muhimu zaidi ni maji.

Kunywa kiasi cha kutosha cha maji kuzimua mkojo na usile kupita kiasi, pia punguza mkusanyiko wa bakteria kwenye kinywa. Hayo yanaweza kusaidia kuzuia aina hizi za mawe.

Katika kesi ya mawe ya koo (mafindofindo), usafi wa mdomo, ikiwa ni pamoja na kusafisha meno mara kwa mara, kunaweza pia kusaidia kupunguza hatari.

Kuzingatia mlo ni jambo muhimu, hasa mawe ya kwenye nyongo, ambayo yanaweza kusababishwa na chakula chenye mafuta sana au unene.

Kuna baadhi ya sababu ambazo haziwezi kuepukika, kama vile kuwa na umri wa zaidi ya miaka 40. Huongeza uwezekano wa kutokea kwa vijiwe vya nyongo.

Pia kuepuka, vyakula vyenye kalsiamu na chumvi nyingi, kama vile maziwa na spinachi, kunaweza kusaidia kuzuia mawe kwenye figo.

Lakini nini kitatokea ikiwa tayari una jiwe? Ikiwa litakufanya ujihisi vibaya, linaweza kuondolewa kwa upasuaji.

Katika kesi ya mawe kwenye figo, unaweza kusubiri hadi mawe yapite kwenye ureta kwenda kwenye kibofu cha mkojo, na kutolewa nje wakati wa kukojoa.

Mawe ya mate mwingine yanaweza kuondolewa kwa kula limau. Mawe ya kooni yanaweza kuondolewa kwa upole na kifaa maalumu.

Kwa muhtasari, kuna matibabu mengi tofauti yanayopatikana kwa aina tofauti za mawe na kuna hatua cha kuchukua za kila siku ambazo zinaweza kusaidia kupunguza hatari ya kutokea mawe.

Pia unaweza kusoma
  • Kipi hutokea miilini mwetu tunapoumizwa na mapenzi?

  • Je, ni vyakula gani husababisha na kupunguza kiungulia?

Imetafsiriwa na Rashid Abdalla

Miili yetu hutoa mawe ya aina gani na tunawezaje kuyazuia? - BBC News Swahili (2024)
Top Articles
Latest Posts
Article information

Author: Carmelo Roob

Last Updated:

Views: 6091

Rating: 4.4 / 5 (45 voted)

Reviews: 92% of readers found this page helpful

Author information

Name: Carmelo Roob

Birthday: 1995-01-09

Address: Apt. 915 481 Sipes Cliff, New Gonzalobury, CO 80176

Phone: +6773780339780

Job: Sales Executive

Hobby: Gaming, Jogging, Rugby, Video gaming, Handball, Ice skating, Web surfing

Introduction: My name is Carmelo Roob, I am a modern, handsome, delightful, comfortable, attractive, vast, good person who loves writing and wants to share my knowledge and understanding with you.